UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA KILIO CHETU.
JINA LA TAMTHILIA :
KILIO CHETU
MWANDISHI : MEDICAL AID FOUNDATION
WACHAPISHAJI : MKUKI NA NYOTA PUBLISHER
MWAKA : 1995
Kilio chetu ni tamthiliya inayovunja ukimya uliotawala miongoni mwa jamii katika kutatua matatizo makubwa ambayo chimbuko lake ni mahusiano ya kijinsia.Katika tamthiliya hii vijana wanatoa sauti ya jitimai iliyojaa sononeko na shutuma dhidi ya wazazi, walezi na viongozi ambao wanafumbia macho suala hili nyeti. Ndiyo maana tamthiliya hii inasisitiza sana haja ya kuwapa vijana elimu juu ya mahusiano ya kijinsia badala ya hofu na vitisho ambavyo vimedhihirika kupitia hali halisi ya kuwa vimeshindwa.

No comments:
Post a Comment