WAHUSIKA
JOTI
- Mhusika mkuu
- Hana elimu
ya jinsia na mahusiano
- Anajiingiza
katika mahusiano ya kimapenzi na wasichana wengi. Wengine wakiwa wakubwa kuliko
yeye.
- Mwisho
anakufa kwa UKIMWI
SUZI
- Mhusika mkuu
- Hana elimu
ya jinsia na mahusiano
- Anajiingiza katika mahusiano ya
kimapenzi na mwanafunzi mwenzake Joti, pia anaambukizwa UKIMWI na kupata mimba.
ANNA
- Msichana
mwenye elimu ya jinsia na mahusiano
- Anakataa
vishawishi vya wanaume kwa sababu anajitambua kwa sababu ya kuwa na elimu ya
jinsia
MAMA SUZI
- Anashikilia
mila na tamaduni za zamani
- Haungi mkono
kuwapatia watoto elimu ya jinsia na mahusiano, anaamini kufanya hivyo ni
kuwaharibu watoto
MJOMBA
- Mwanaume mtu
mzima
- Anaunga
mkono wazazi kuwapatia watoto wao elimu ya jinsia na mahusiano.
Wahusika wengine ni; Baba joti, Mama Joti, Baba Anna, Choggo,
Mwarami, Jumbe, Chausiku, Jirani, na wengineo.
MANDHARI
Mandhari ya mjini yametumiwa na mwandishi. Pia kunayo mandhari
ya;
Nyumbani, kijiweni, barabarani, n.k
No comments:
Post a Comment