UCHAMBUZI WA VIPENGELE VYA FANI KATIKA TAMTHILIYA YA KILIO
CHETU
MUUNDO
Tamthiliya hii imetumia muundo wa moja kwa moja. Inaanza kwa
kutuonesha wazazi wakibishana juu ya kutoa elimu ya jinsia na mahusiano. Mwisho
Joti mtoto ambaye hakupatiwa elimu hiyo anampa mimba mtoto mwenzake Suzi.
Baadae Joti anakufa kwa UKIMWI.
Pia tamthiliya hii imegawanywa katika sehemu sita.
sehemu ya kwanza. Inaonesha jinsi ambavyo gonjwa la UKIMWI
linaiteketeza, jamii wengi wao wakiwa watoto ambao hawakuwa na elimu ya jinsia
na mahusiano.
sehemu ya pili. Wazazi wanabishana juu ya kuwapatia elimu ya
jinsia na mahusiano watoto wao. Mama Suzi anasema jambo hilo liko kinyume na
maadili, lakini Baba Anna yeye anaunga mkono suala hilo.
sehemu ya tatu. Inaeleza kuhusu watoto Joti na Suzi ambao
wamekwisha anza mambo ya ngono. Pia watoto wameathiriwa na utandawazi kwani
wanaangalia video za ngono bila wasiwasi.
Sehemu ya nne. Inazungumzia tabia hatarishi za Joti kuwa na
wasichana wengi. Vilevile Anna kutokana na elimu ya jinsia na mahusiano
aliyonayo, anaendelea kukwepa vishawishi.
Sehemu ya tano. Mtoto Suzi kapata mimba, anabaki njia panda
akiwa hajui afanye nini.
Sehemu ya sita. Tunamuona Joti akifa kwa UKIMWI, na Suzi
anabaki akiwa na mimba pamoja na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
MTINDO
Tamthiliya hii imetumia mtindo wa;
i.
Dayolojia – majibizano ya wahusika yametawala toka mwanzo mpaka mwisho
wa tamthiliya hii.
ii.
Monolojia – mtindo huu wa masimulizi umetumika japo kwa kiasi kidogo.
iii. Mtindo
wa masimulizi ya ki ngano - mfano katika ukurasa wa 1 Mtambaji anasimulia,
“Hapo zamani za kale
paliondokea kisiwa kimoja kikubwa sana. Kisiwa kilikuwa na watu wa kila aina…”
iv. Matumizi
ya nyimbo – katika ukurasa wa 29, Anna anaimba wimbo unaokemea wanaume wanaomfuata
kumlaghai.
“Anna, Anna, Anna
mie niacheni mie x 2
Msichana mdogo bado ninasoma niacheni mie.”
v. Matumizi
ya nafsi
Nafsi zote zimetumika lakini nafsi ya pili imetawala zaidi.
No comments:
Post a Comment